UVIMBE KWENYE KIZAZI,SABABU ZAKE, DALILI ZAKE NA TIBA YAKE ASILI
TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI,SABABU, DALILI NA TIBA YAKE ASILI FIBROID NI NINI? Siku hizi kuna ongezeko kubwa sana la huu ugonjwa hebu tega sikio. Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi. Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi. Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke. Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’. Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu . SABABU ZA MWANAMKE KUPATA UVIMBE