SABABU KUU 5 ZINAZOWEZA KUSABABISHA UWE NA TUMBO KUBWA (Abdominal distension)
SABABU KUU 5 ZINAZOWEZA KUSABABISHA UWE NA TUMBO KUBWA (Abdominal distension)
PANDEX HERBAL CLINIC
+255 656 198 441
pandexclinic@gmail.com
DAR ES SALAAM, ILALA
⚫ Zipo sababu kuu 5 zinazoweza kusababisha mtu akaonekana kuwa na tumbo kubwa kama ifuatavyo;⤵️⤵️
1. 🔗 Tumbo kujaa gesi (Flatus). Watu wengi wamekuwa na matumbo makubwa wakidhani kwamba wana vitambi vinavyotokana na mafuta kumbe matumbo yao yamejaa gesi inayosababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa choo na kuwa na Acid reflux.
2. 🔗 Tumbo kujaa kinyesi (Faeces). Kwa wale ambao hawapati choo inavyotakiwa (Constipation) hujaa matumbo yao kana kwamba wana vitambi vya mafuta ilihali matumbo yamejaa kinyesi (Mavi) hali ambayo inasababisha waonekane kuwa na matumbo makubwa.
3. 🔗 Mimba (Fetus). Hii ni maalumu kwa wanawake kwani wao ndio wana uwezo wa kupata mimba hivyo hupelekea matumbo yao kuwa makubwa kutokana na uwepo wa mtoto tumboni.
4. 🔗 Tumbo kujaa maji (Fluid/Ascites). Tumbo (Abdomen) huweza kujaa maji kutokana na sababu mbalimbali kama vile magonjwa mbalimbali ikiwemo Magonjwa ya Ini na Figo hali inayopelekea tumbo kujaa na kuonekana kama ni mtu mwenye kitambi.
5. 🔗 Tumbo kuwa na mafuta mengi(Fat).Hii ni kutokana na mtindo mbaya wa maisha ikiwemo kutofanya mazoezi, kula sana vyakula vya wanga na Sukari pamoja na vinywaji vyenye sukari hali inayopelekea tumbo kujaa mafuta kwani kila kiasi cha Sukari kinapozidi mwili hukibadili na kuwa Mafuta kisha mafuta hayo huhifadhiwa kwenye mwili wako ikiwemo kwenye tumbo (Abdomen).
KUMBUKA:⤵️⤵️
⚫ Kutopata choo inavyotakiwa ni katika visababishi vikubwa vya kupata saratani ya Utumbo lakin pia kutopata choo ni katika VIASHIRIA vya Saratani ya Utumbo hivyo usipuuzie.
⚫ Kama wewe una tumbo kubwa basi kabla ya kuanza kuwaza kwamba una mafuta mengi, angalia kwanza upati wako wa choo,je unapata choo inavyotakiwa? Je tumbo lako lina Gesi nyingi? Je Una Acid reflux? Je una Hernia?.Je una magonjwa ya ini na Figo?.Kisha fanya maamuzi baada ya kujua chanzo cha wewe kuwa na tumbo kubwa(Abdominal distension).
KWA USHAURI NA MATIBABU:⤵️⤵️
PANDEX HERBAL CLINIC
+255 656 198 441
pandexclinic@gmail.com
DAR ES SALAAM, ILALA
TANZANIA.
Comments
Post a Comment